Header Ads

Breaking News

SIMULIZI

PATA SIMULIZI KALI NA ZA KUSISIMUA:

SINA WA KUMLILIA
  Hii ni simulizi ya kusisimua na yenye kuelimisha, simulizi hii imetungwa na Geophrey Sanga. isome simulizi hii uweze kujifunza mengi

  1. kwa sehemu ya kwanza ya simulizi bonyeza hapa
  2. kwa sehemu ya pili ya simulizi bonyeza hapa
  3. kwa sehemu ya tatu ya simulizi bonyeza hapa
MZIMU WA MAMA 

Mzimu wa mama ni simulizi kali inayo husu maisha ya James tangu kifo cha mama yake, amekuwa akipata matatizo mengi sana. Kabla ya kifo cha mama yake James alikuwa anaishi na mama yake pamoja na wadogo zake kwa raha na amani. lakini baada ya kifo cha mama yake, James ammekuwa akipata matatizo mengi sana. fuatilia kwa ukaribu kisa hiki ujue ni kitu gani kimesababisha James apate matatizo na kwa nini simulizi hii iitwe mzimu wa mama. ungana na Jemes akisimulia kisa hiki.


                                                        *SIMULIZI SEHEMU YA KWANZA*
Kabla ya kifo cha mama yangu tulikuwa tukiishi mimi, mama yangu pamoja na wadogozangu wawili, baada ya baba yangu kufariki kwa ajari mbaya ya gari. Baba yangu aligogwa na gari akiwa ametoka  sokoni kwani tuliku na kibada kidogo tulichokuwa tunauza bidhaa mbalimbali. Baada ya kifo cha baba tuliendelea kuishi mimi na mama pamoja na wadogozangu. Nilihitimu darasa la saba sikupata bahati ya kuendelea na masomo ya sekondali hivyo nililazimika kubaki nyumbani nikimsaidia mama yangu kuuza kibandani.

Tuliendelea kuisha na mama kwa amani na furaha kwani mama alijitahidi kwa kila namna kutufanya tuwe na furaha. siku moja jioni mama yangu alikuwa anapika jikoni ghafla nikasikia sauti “James” aliita kwa nguvu sana hajawahi kuniita hivyo hata siku moja. Nilishituka sana, nikakimbia kuelekea jikoni nikakuta mama anagalagala chini.
                     “mama, mama, mamaaaa!”
Nilijaribu kuita lakini hakuweza kunijibu chochote alikuwa akigalagala tu na kugeuza macho huku na kule. Baadaye akatamuka maneno kwa shida sana, “na...na..omba....wa....ite wa do..go zakooooo!” akavuta sauti kwa upole uku akiwa amenishikilia mikono yangu kifuani kwake alionesha amebanwa na kifua kama mgonjwa wa pumu.

Nikawaita wadogo zangu, mkubwa akaja haraka mdogo akabaki alikuwa akicheza kwa majirani,
 “...haraka kimbia neenda kawaite majirani pamoja na mdogo wako mje haraka ...” nili mwamuru kwa nguvu.
Majirani wakaja haraka kwani mdogo wangu alikimbia kuwafuata huku akiogopa sana nahisi ndo sababu ya majirani kufika mapema nyumbani. Wadogo zangu wakasogea karibu na mama akawashika mikono huku akigeuza geusa macho. Majirani wakahangaika sana hawakujua nini cha kufanya. Ghafla mama akatoa sauti huku akitushikilria mikono kwa nguvu “kwa... her..iiiii!” “mamaaaaaaaaaaa”  niliita kwa nguvu. Lakini mama alikuwa hawezi tena kunisikia kwani roho yake iliacha mwili, pumzi ika piga mbizi na milango ya fahamu ikafunga. Kilifuata kilio tu hatujui tufanyeje? Jirani mmoja akaja akamziba macho aliyokuwa ameangalia juu akiiangalia dunia mara ya mwisho akiwa anashusha pumzi na kuiaga dunia kwa huzuni.

kilio tupu kilitanda sio majirani sio mimi sio wadogo zangu........tulilia sana hatukujua ni nini kimemsibu mama yetu kwani alikuwa mzima tu hakulalamika kuumwa. hatukuwa na jinsi kwan mungu ndo alipanga iwe hivyo.
Siku ya pili yake taratibu za mazishi ziliendelea, baada ya mazishi tukaendelea na matanga. Baada ya wiki moja ndugu na wana ukoo wote wakaamuru kuanua matanga na kugawa majukumu ya kusimamia mali za marehemu mama yetu pamoja na jinsi ya kutulea sisi.

Ndugu walishauri turudi tukaisha na bibi kijijini, Ili tuwe cini ya uangalizi wa bibi kwani hatukuwa na uwezo wa kijitegemea.

Mikakati ya kuhamia kijijini iliendelea, tukahamia kijijini. Tukayazoea maisha ya kijijini ingawa mwanzo yalitupa shida sana mimi na wadogozangu pia, Lakini baada ya mwezi mmja tulikuwa tumeyazoea maisha ya kijijini.
**BAANA YA MIEZI MIWILI**
Baada ya miezi miwili kukaa kijijini na kuyazoea zaidi maisha ya kijijini, siku moja usiku nikiwa nimelala nikasikia sauti ikiniita  “Jamessssssssss.............Jamessssssssss.......Jamessiiiiiiiii!....” sauti ilisikia ikiwa na mwangwi wa mtetemeko. Nilishituka kwa sana, kwa sababu ulikuwa usiku wa manane, lakini nilipo angalia huku na huku sikuona mtu yeyote aliye niita, nikajaribu kuinuka kitandani nikijua labda bibi yangu alikuwa akiniita laikini niliposogelea mlango wa bibi nikakuta anakoloma tu kwa usingizi mzito. Nikahisi labda nilikuwa naota, Nikarudi kulala. Kabla sijapata usingizi ghafla nikasikia suti tena iliyoita kwa nguvu “....James....” iliita kwa nguvu hadi masikio yaliuma nikaisi kama masikio yalitaka kupasuka, nikashituka na kupiga kelele kwa nguvu
 “heeeeeeeeee!” 
Bibi alisikia makelele yangu alishituka kutoka usingizini.
       “James kuna nini?”
            “Mimi sijui..!” kwa woga nikajibu.
            “Hujui nini mbona unapiga makelele”
Nikamjibu bibi yangu wa hasira na uoga huku nikilia. Mara bibi akaja chumbani kwangu, tukatoka sebureni, nikamweleza jinsi nilivyo yasikia makelele yale.
“ usijari ulikuwa unaota tu. Nenda rudi ukalale.” bibi akanitia moyo
Nikarudi kulala nikiwa bado siamini kilichotokea.
“Huu ni mzimu au ni kitu gani?”
Nilijiuliza maswali mengi kwani nisha wahi kusikia kuwa mizimu huwa mara nyingi ikitaka kumtokea mtu basi hutokea usiku wa manane. Lakini pia nika jipa moya, huenda ni malaika anataka kusema nami kwani nisha wahi kusoma kitabu cha daniel anaeleza jinsi alivyoitwa na mungu nikajifariji, na kujilaumu kwa nini sikuitika, mungu pia husema na watu wake usiku wa manane.
Usiku mzima nilikuwa nawaza sikupata majibu ya haraka hadi kulipo kalibia kupambazuka ndipo nikapata kausingizi kaliko nibembeleza hadi saa moja asubuhi  wakati ambapo bibi yangu aliniamsha kunijulia hali.

     "..James..."
     ...naam....
      "umeamkaje"
      salama tu bibi.
baada ya bibi kunijulia hali akaondoka na kwenda kuendelea na shughuli zake za kila siku.

Mchana mzima nilikuwa nikiwaza kilichotokea lakini sikupata majibu. Usiku ukaingia tena baada ya chakula cha usiku kila mtu aliaga na kuelekea chumbani kwake kulala. Nilipokuwa naingia chumbani ghafla nikaona mwanga na mtu amekaa kitandani kwangu akiwa amevalia shuka jekundu kajitanda kichwa kizima na mikononi akiwa ameshika kitu cha mvilingo kama dunia, mikono yake ilikuwa na kucha ndefu.    
            "mamaaaaaa........!!!"
            "James....... james....nini?........................itaendelea siku njingine
 


usikose kufuatilia siku nyingine ujue nini kilimtokea james na ilikuwaje.endelea kuwa nasi

No comments