Header Ads

Breaking News

KARIBU SEHEMU YA TATU YA SIMULIZI YETU YA KUSISIMUA: SINA WA KUMLILIA

  1. Sehemu ya kwanza ya simulizi bonyeza hapa
  2. Sehemu ya pili ya simulizi bonyeza hapa.

ILIPOISHIA.
Tuliona sehemu ya pili ya simulizi hii baada ya kifo cha baba yake msibani kila mtu alimchukia. sasa tuendelee kufuatilia kipi kilitokea baada ya hapo.

Nikiwa msibani kila mtu alinichukia, sikuwa na jinsi maana makosa yote niliyafanya mimi hadi magazeti yaliandika taarifa zangu. wengine walinitupia magazeti ili niyasome, yalikuwa na vichwa vikali na vizito mno.
MALAYA ALIYEGONGANISHA WANAUME YAMEMTOKEA PUANI. Niliacha kuhuzunika msiba wa baba sasa nilihuzunika kwa aibu iliyo nikuta.

msiba ukamalizika tukaanua matanga, wakati wa kuanua matanga na kumtafuta mridhi wa mali za baba atakaye saidia kuziendesha hakuna aliye kubali kwani siku ya msiba risala ilisomwa baba alionekana alikuwa na deni kubwa sana benk. kila mtu alikwepa kulibeba deni hilo. haikuishia hapo tu, kila mtu alikataa kuishi na mimi, kila mmoja alisema siwezi kuishi na maraya huyu.niliumia sana. nikaachwa peke yangu kwenye jumba lililokuwa na deni kubwa benki.

Baada ya miezi sita kupita benki hawakupata malipo ya miezi mitatu ya deni la baba yangu, haikuwa shida kwao wakafika nyumbani na kunitaka nifike ofisini kwao. siku iliyo fuata wakanitaka niwe tayari kulipa malipo na ikishindikana watapiga mnada nyumba ya baba yangu.

Na wakati huo benki wananisumbua ndugu msomaji maisha yangu yalikuwa magum sana sikuwa na msaada wowote maana nilizoea kupewa kila kitu na baba yangu, sikujua kufanya biashara, wala kujishughulisha na kitu chochote. sikuwa na njia yoyote ya kupata pesa, hata pesa ya kula niliipata kwa shida. mda mwingine nkawalilia wazazi wangu kwanini walinidekeza vile, kwanini hawakutuzaa wawili tungesaidiana. nitaishije mimi.

 Watu walinicheka kila sehemu niliyo pita, alikuwa anajiona sister duu mbana sasa amechakaa. Hakuna mwanaume aliye nipenda tena baada ya ile skendo. Baada ya mwezi mmoja benki wakaja kupiga mnada nyumba kwani makubaliano ilikuwa ni ndani ya mwezi mmoja niwe nimelipa malimbikizo ya madeni ya mwezi sita.

Nyumba ikauzwa sikuwa na pakuenda kila ndugu yangu hakunitaka tena. rafiki yangu mmoja aliyekuwa anaishi katika nyumba ya kupanga alinisaidia na kuniambia nikaishi naye. Maisha mapya ndipo yakaanza upya, sikufikilia kuishi katika nyumba za kupanga hata siku moja. Ndugu msomaji maisha yalikuwa magumu sana. Tulifanya biashara ya kuuza vyakula gengeni mda mwingine vyakula viliisha mda mwingine vyakula vilibaki na tukaishia kuvigawa bule au kuvimwaga tu. sikufikiria hata siku moja kuwa ninge wahi fanya biashara kama hii.

siku moja nikiwa jioni rafiki yangu alichukuliwa na rafiki yake wakaondoka na kuniacha peke yangu. siku hizo tulikuwa hatuna biashara tena kwani mtaji wote ulikufa, tulijaribu kutafuta kila njia ilishindikana. alipo ondoka akarudi asubuhi, sikuweza kumuliza nkajua alilala kwa rafiki yake. alifanya hivyo sasa kwa mda wa wiki sasa na kila akirudi alikuwa anarudi na pesa nzuri tu, sasa nikapata wasiwasi sijui anaenda kuiba au ndo rafiki yake anampatia.

Siku moja rafiki yangu akaniambia, sasa tunatakiwa kusaidiana kazi maana wote ni wanawake hakuna mwanaume hapa sote tuwe na njia ya kutafuta pesa. sasa ntapata wapi na biashara ndo zinagoma. jioni akaniambia niende kwa rafiki yake ili akanifundishe kazi. kufika huko nikaingizwa kwenye chumba maalum. huko kulikuwa na dhana na vifaa mbalimbali tayari kwa kazi. nikapewa neno moja utayari wako tu, tena unafaa kwa biashara hii. Heeeeee................................... ITAENDELEA

USIKOSE KUFUATILIA SEHEMU YA NNE NA YA MWISHO YA SIMULIZI HII
Kila mtu alinichukia hata ndugu zangu walinichukia, nilifedheheka sana. Hapo ndipo maisha yangu yalipo anzia kupoteza mwelekeo.....

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
Kila mtu alinichukia hata ndugu zangu walinichukia, nilifedheheka sana. Hapo ndipo maisha yangu yalipo anzia kupoteza mwelekeo

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt
Kila mtu alinichukia hata ndugu zangu walinichukia, nilifedheheka sana. Hapo ndipo maisha yangu yalipo anzia kupoteza mwelekeo

Copy and WIN : http://ow.ly/KfYkt

No comments