SIMULIZI
SINA WA KUMLILIA
Hii ni simulizi ya kusisimua na yenye kuelimisha, simulizi hii imetungwa na Geophrey Sanga. isome simulizi hii uweze kujifunza mengi
- kwa sehemu ya kwanza ya simulizi bonyeza hapa
- kwa sehemu ya pili ya simulizi bonyeza hapa
- kwa sehemu ya tatu ya simulizi bonyeza hapa
Mzimu wa mama ni simulizi kali inayo husu maisha ya James tangu kifo cha
mama yake, amekuwa akipata matatizo mengi sana. Kabla ya kifo cha mama yake James alikuwa anaishi na mama yake pamoja na
wadogo zake kwa raha na amani. lakini baada ya kifo cha mama yake, James
ammekuwa akipata matatizo mengi sana. fuatilia kwa ukaribu kisa hiki ujue ni kitu gani kimesababisha James apate matatizo na kwa nini simulizi hii iitwe mzimu wa mama. ungana na Jemes akisimulia kisa hiki.
*SIMULIZI SEHEMU YA KWANZA*
Kabla ya kifo cha mama yangu tulikuwa tukiishi mimi, mama yangu pamoja na
wadogozangu wawili, baada ya baba yangu kufariki kwa ajari mbaya ya gari. Baba
yangu aligogwa na gari akiwa ametoka sokoni
kwani tuliku na kibada kidogo tulichokuwa tunauza bidhaa mbalimbali. Baada ya
kifo cha baba tuliendelea kuishi mimi na mama pamoja na wadogozangu. Nilihitimu
darasa la saba sikupata bahati ya kuendelea na masomo ya sekondali hivyo
nililazimika kubaki nyumbani nikimsaidia mama yangu kuuza kibandani.
Tuliendelea kuisha na mama kwa amani na furaha kwani mama alijitahidi kwa kila namna kutufanya tuwe na furaha. siku moja
jioni mama yangu alikuwa anapika jikoni ghafla nikasikia sauti “James” aliita
kwa nguvu sana hajawahi kuniita hivyo hata siku moja. Nilishituka sana,
nikakimbia kuelekea jikoni nikakuta mama anagalagala chini.
“mama, mama,
mamaaaa!”
Nilijaribu kuita lakini hakuweza kunijibu chochote alikuwa akigalagala tu na kugeuza macho huku na kule.
Baadaye akatamuka maneno kwa shida sana, “na...na..omba....wa....ite wa do..go
zakooooo!” akavuta sauti kwa upole uku akiwa amenishikilia mikono yangu kifuani kwake alionesha amebanwa na kifua kama
mgonjwa wa pumu.
Nikawaita wadogo zangu, mkubwa akaja haraka mdogo akabaki alikuwa akicheza
kwa majirani,
“...haraka kimbia neenda kawaite majirani pamoja na mdogo wako
mje haraka ...” nili mwamuru kwa nguvu.
Majirani wakaja haraka kwani mdogo wangu alikimbia kuwafuata huku akiogopa
sana nahisi ndo sababu ya majirani kufika mapema nyumbani. Wadogo zangu
wakasogea karibu na mama akawashika mikono huku akigeuza geusa macho. Majirani
wakahangaika sana hawakujua nini cha kufanya. Ghafla mama akatoa sauti huku
akitushikilria mikono kwa nguvu “kwa... her..iiiii!” “mamaaaaaaaaaaa” niliita kwa nguvu. Lakini mama alikuwa hawezi
tena kunisikia kwani roho yake iliacha mwili, pumzi ika piga mbizi na milango
ya fahamu ikafunga. Kilifuata kilio tu hatujui tufanyeje? Jirani mmoja akaja
akamziba macho aliyokuwa ameangalia juu akiiangalia dunia mara ya mwisho akiwa
anashusha pumzi na kuiaga dunia kwa huzuni.
kilio tupu kilitanda sio majirani sio mimi sio wadogo zangu........tulilia sana hatukujua ni nini kimemsibu mama yetu kwani alikuwa mzima tu hakulalamika kuumwa. hatukuwa na jinsi kwan mungu ndo alipanga iwe hivyo.
Siku ya pili yake taratibu za mazishi ziliendelea, baada ya mazishi tukaendelea na matanga.
Baada ya wiki moja ndugu na wana ukoo wote wakaamuru kuanua matanga na kugawa
majukumu ya kusimamia mali za marehemu mama yetu pamoja na jinsi ya kutulea sisi.
Ndugu walishauri turudi tukaisha na bibi kijijini, Ili tuwe cini ya
uangalizi wa bibi kwani hatukuwa na uwezo wa kijitegemea.
Mikakati ya kuhamia kijijini iliendelea, tukahamia kijijini. Tukayazoea
maisha ya kijijini ingawa mwanzo yalitupa shida sana mimi na wadogozangu pia,
Lakini baada ya mwezi mmja tulikuwa tumeyazoea maisha ya kijijini.
**BAANA YA MIEZI MIWILI**
Baada ya miezi miwili kukaa kijijini na kuyazoea zaidi maisha ya kijijini, siku moja usiku nikiwa nimelala nikasikia sauti
ikiniita
“Jamessssssssss.............Jamessssssssss.......Jamessiiiiiiiii!....” sauti
ilisikia ikiwa na mwangwi wa mtetemeko. Nilishituka kwa sana, kwa sababu ulikuwa usiku wa manane, lakini nilipo
angalia huku na huku sikuona mtu yeyote aliye niita, nikajaribu kuinuka
kitandani nikijua labda bibi yangu alikuwa akiniita laikini niliposogelea
mlango wa bibi nikakuta anakoloma tu kwa usingizi mzito. Nikahisi labda
nilikuwa naota, Nikarudi kulala. Kabla sijapata usingizi ghafla nikasikia
suti tena iliyoita kwa nguvu “....James....” iliita kwa nguvu hadi masikio
yaliuma nikaisi kama masikio yalitaka kupasuka, nikashituka na kupiga kelele
kwa nguvu
“heeeeeeeeee!”
Bibi alisikia makelele yangu alishituka kutoka usingizini.
“James kuna nini?”
“Mimi
sijui..!” kwa woga nikajibu.
“Hujui nini mbona unapiga
makelele”
Nikamjibu bibi yangu wa hasira na uoga huku nikilia. Mara bibi akaja chumbani
kwangu, tukatoka sebureni, nikamweleza jinsi nilivyo yasikia makelele yale.
“ usijari ulikuwa unaota tu. Nenda rudi ukalale.” bibi akanitia moyo
Nikarudi kulala nikiwa bado siamini kilichotokea.
“Huu ni mzimu au ni kitu gani?”
Nilijiuliza maswali mengi kwani nisha wahi kusikia kuwa mizimu huwa mara
nyingi ikitaka kumtokea mtu basi hutokea usiku wa manane. Lakini pia nika jipa moya,
huenda ni malaika anataka kusema nami kwani nisha wahi kusoma kitabu cha daniel
anaeleza jinsi alivyoitwa na mungu nikajifariji, na kujilaumu kwa nini
sikuitika, mungu pia husema na watu wake usiku wa manane.
Usiku mzima nilikuwa nawaza sikupata majibu ya haraka hadi kulipo kalibia
kupambazuka ndipo nikapata kausingizi kaliko nibembeleza hadi saa moja asubuhi wakati ambapo bibi yangu aliniamsha kunijulia hali.
"..James..."
...naam....
"umeamkaje"
salama tu bibi.
baada ya bibi kunijulia hali akaondoka na kwenda kuendelea na shughuli zake za kila siku.
Mchana mzima nilikuwa nikiwaza kilichotokea lakini sikupata majibu. Usiku
ukaingia tena baada ya chakula cha usiku kila mtu aliaga na kuelekea chumbani
kwake kulala. Nilipokuwa naingia chumbani ghafla nikaona mwanga na mtu amekaa
kitandani kwangu akiwa amevalia shuka jekundu kajitanda kichwa kizima na
mikononi akiwa ameshika kitu cha mvilingo kama dunia, mikono yake ilikuwa na
kucha ndefu.
"mamaaaaaa........!!!"
"James....... james....nini?........................itaendelea siku njingine
usikose kufuatilia siku nyingine ujue nini kilimtokea james na ilikuwaje.endelea kuwa nasi
No comments