Header Ads

Breaking News

Lowassa ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Image result for lowassa
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameitwa na Ofisi ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz.
Lowassa akizungumza na Mwananchi leo (Jumatatu), amesema ameitwa kwa DCI lakini hajui anachoitiwa.

Hata hivyo, amesema anahisi ni kauli yake kuhusu mashehe wa kikundi cha Uamsho cha Zanzibar wanaoshtakiwa kwa tuhuma ya ugaidi.

 “Ni kweli nimetakiwa niripoti kesho saa 4:00 asubuhi katika ofisi ya DCI. Sijui wananiitia nini, lakini nahisi ni kuhusu nilichosema kuhusu mashehe wa Uamsho,” amesema Lowassa.

Jana katika taarifa kwa vyombo vya habari, Lowassa alikaririwa akiitaka serikali kuwaachia huru mashehe hao wanaoshikiliwa kwa zaidi ya miaka minne sasa.

Taarifa hiyo ilisema Lowassa alitoa ombi hilo alipozungumza katika futari iliyoandaliwa na mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara.

PATA HABARI HIZI FACEBOOK NA WHATSAPP 
BONYEZA VITUFE HIVI KUJIUNGA
Image result for whatsapp FACEBOOK

No comments