Header Ads

Breaking News

Waziri Mwakyembe akanusha habari ya gazeti la Dira lililosema ametapeli bilioni 2

 Waziri wa katiba na sheria Harrison Mwakyembe amekanusha taarifa za uongo zilizotolewa na gazeti la DIRA, Habari iliyokuwa ikimuhusisha utapeli bilioni 2. Pia ameahidi kuwapeleka Mahakamani wahusika wote waliosambaza taarifa hiyo bila kuwa na ushahidi.




Akitoa taarifa hizo kwa vyombo vya habari mheshimiwa Mwakyembe aliseme
" Jumatatu ya tarehe 13/6/2016 gazeti la DIRA YA MTANZANIA lilichapisha taarifa iliyosema Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2, kupandishwa mahakamani wakati wowote. Napenda nikiri kuwa sijawahi kushuhudia upotoshaji mkubwa na wa makusudi kama huu 
Ukiisoma taarifa za gazeti hili utaona waziwazi umakini na weredi wa uandishi wa habari unakosekana, hata jina la wizara yangu limekosewa. Makosa yaliyonukuliwa na gazeti hili ni makosa ya jinai kwahiyo nahakika Dira wanauhakika ni lini Polisi walinihoji
 
Wameona hiyo haitoshi, wiki hii wamekuja na taarifa ya kulizalilisha jeshi letu kwa kusema kifaru chake cha kiviti kimeibwa, huku ni kukosa uzalendo na kulitia doa jeshi letu. Tukikaa kimya tutaambiwa tena kuwa hicho kifaru kinatumika kama daladala.
Tutafungua kesi hii mahakama kuu ya Tanzania na bado mimi na mawakili wangu tunaangalia impact na kuhusika kwa vyombo vikubwa vya  habari  kama ITV na Star Tv  kwa kutangaza taarifa "


KAMA ULIPITWA NA HABARI HIZI SOMA HAPA

Wabunge wa ukawa watoa kituko bungeni

Werikari yasitisha ajira zote 

Harmonize na wolper penzi lazidi kupamba moto
Harmonize na Jackline Wolper penzi lazidi kupamba moto Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

Make Money Online : http://ow.ly/KNICZ

No comments