Header Ads

Breaking News

UCHAMBUZI WA HABARI ZA MAGAZETINI LEO 26/06/2012

Habari kubwa iliyo shika head line za magazeti yote ya tanzania ni ile inayosema MAGUFULI AWAPA RUNGU POLISI ingawa imeandikwa kwa namna tofauti tofauti. hapa tunakuletea habari hii kama ilivyo andikwa na gazeti la HABARI LEO


 Magufuli awapa rungu Polisi

RAIS John Magufuli amewataka polisi kujiongeza katika utendaji kazi wao bila kusubiri majambazi kufikia hatua ya kuwanyang’anya silaha katika vituo au kuvamia nyumba, watu na kuwanyang’anya mali zao.

Aidha, alisema umefikia wakati wa polisi sasa kugangamala na kutosita kuwanyang’anya majambazi silaha haraka na akiwataka kutumia mbinu za medani kwani wananchi wamechoka kutafuta mali zao huku watu wengine wakija kuchukua na kuahidi kuangalia namna ya kuwanunulia helikopta kwa ajili ya doria.

Magufuli alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akizindua mpango wa usalama wa raia katika kuboresha utendaji kazi kwa kutumia Mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) awamu ya pili unaoanza kutekelezwa katika wilaya ya Kinondoni Julai mosi mwaka huu na baadaye kusambaa nchi nzima baada ya miaka mitatu na kupunguza uhalifu kwa asilimia 10 kila mwaka.


“Kama mnazo bunduki za kutosha kwa nini jambazi aondoke bila kunyang’aywa silaha anayotumia haraka haraka ,ninaposema haraka haraka mnanielewa, kwa nini jambazi aende mahali akafanye ujambazi na polisi mshindwe kumnyang’anya silaha yake haraka haraka,”==>> MAGUFULI

Chanzo HABARI LEO 26/06/2016

No comments