Header Ads

Breaking News

KOCHA WA YANGA (PLUIJM) ATOA MBINU WATAKAZO ZITUMIA KUWAFUNGA TP MAZEMBE


Image result for yanga image

YANGA imerejea kutoka kambini Antalya, Uturuki huku Kocha Mkuu, Hans Pluijm akiahidi kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo keshokutwa. 

Akizungumza jana, Pluijm alisema kambi ya mazoezi nchini Uturuki imewajenga na ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri Jumanne wakati Yanga itakapocheza na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).



“Nawajua TP Mazembe, ni timu nzuri ina wachezaji ambao wamecheza nchi mbalimbali na baadhi yao nawafahamu nilishawafundisha nikiwa Ghana. “Mchezo utakuwa mgumu na mzuri, naamini mashabiki pamoja na kuwa tunasaka pointi tatu, tutawapa burudani, ” ==>> Pluijm.

Alisema wamefanyia kazi udhaifu uliojitokeza katika mchezo wao wa kwanza na MO Bejaia Jumapili na kwamba ni jukumu la wachezaji kubadilika kwa kucheza kutokana na maelekezo yake.

Kwa upande wake akizungumza jana, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro alisema maandalizi yanaenda vizuri ya mchezo huo na kwambaba kiingilio cha chini kitakuwa Sh. 7,000 wakati kingilio cha juu ni Sh 30,000.

Image result for yanga image

No comments