Header Ads

Breaking News

MASHABIKI WA YANGA KUINGIA BURE MECHI YA YANGA NA TP MAZEMBE

 Image result for MASHABIKI YANGA IMAGE

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeamua mashabiki watakaoingia uwanjani kushuhudia mechi kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe, kesho Jumanne hawatalipa viingilio.

Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho inayosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa Yanga, sasa ni bure. Ikiwa hilo litatekelezeka, Yanga inaweza kupoteza zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zingeweza kupatikana kutokana na kiingilio cha mchezo huo

Akithibitisha ukweli wa taarifa hiyo mwenyekiti wa klabu ya Yanga alisema


Image result for yusuph manji
"Kweli viongozi tumekubaliana kwa umoja baada ya kukaa. Tunataka mashabiki wa Yanga na mashabiki wengine wanaopenda mpira bila kujali ni wa timu gani wakashuhudie mpira." ==>> Manji:

Pia kuhusu suala la kupoteza pesa nyingi ambazo zingekusanywa kwenye mchezo huo alisema
"Yanga ipo kwa ajili ya wananchi, Yanga ni furaha ya watu wengi".==>> Manji:

pia kuhusu kuingia kwa mashabiki ambao si mashabiki wa yanga alisema

"Mashabiki wa Yanga ni wengi sana Tanzania. Bado hatuamini Wacongo wanaweza kuwazidi Watanzania kwa wingi. Hata watu wa Simba ni mashabiki kutoka Tanzania, waende wakaiunge mkono Yanga. Siku moja Yanga watawaunga mkono wao wakiwa wanashiriki michuano ya kimataifa". ==>> Manji

No comments