Header Ads

Breaking News

KAYA MASIKINI TANZANIA ZAPATIWA BILIONI 440

Serikali leo imesaini makubaliano ya nyongeza ya fedha kwa ajili ya mfuko wa maendelea ya jamii TASAF, makubaliano ambayo yataifanya benki ya dunia iipatie Tanzania bilioni 440 kwa ajili ya kupeleka kwenye kaya maskini ikiwa ni chachu ya maendeleo kwa kaya masikini kuwapatia ajira na kuzipa fulsa ya  kuwapeleka watoto wao shule na kupata huduma za afya.
 Image result for kaya masikini
Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile amesaini mkataba huo kwa niaba ya serikali na kusema kuwa katika mwaka huu wa fedha mwaka 2015/2016 serikali na benki ya dunia imepitisha miradi 10 ambayo ina thamani ya trilioni 1.9 ambazo zitapelekwa katika miradi mbalimbali kama kuboresha kilimo, mradi wa kuimarisha umeme vijijini na elimu.
 Image result for kaya masikini         vs Image result for world bank

No comments