Header Ads

Breaking News

WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO MWAKA HUU 2015

BOFYA HAPA KUANGALIA
Baada  ya  wanafunzi waliomaliza  kidato  cha nne mwishoni  mwa mwaka  jana kusubii selection  sasa s
OWM-TAMISEMI Imetangaza majina ya wanafunzi  waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya  Ufundi kwa mwaka 2015. Wanafunzi waliochaguliwa ni kutoka shule za Serikali na zisizo za Serikali.  Jumla ya Wanafunzi 55,003 wakiwemo wasichana 23,303 na  wavulana  31,700 wamechaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi.
Kati ya wanafunzi waliochaguliwa 29,744 wakiwemo wasichana11,450 na wavulana18,294 sawa na asilimia 54.08 watajiunga na masomo ya Sayansi na Hisabati; nawanafunzi 25,259 wakiwemo wasichana 11,853 na wa  vulana13,406 sawa na asilimia 45.92 wamechaguliwa kusoma masomo ya Sanaa na Biashara.Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano mwaka 2015 wataanza muhula wa kwanza tarehe 18 Julai,2015 na hakutakuwa na fursa ya mabadiliko yoyote ya shule.
Wanafunzi wote wanatakiwa kuripoti katika shule walizopangwa kwa wakati. Endapo mwanafunzi atachelewa kuripoti kwa zaidi ya siku 14 kuanzia tarehe ya mwisho ya kuripoti, nafasi yake  itachukuliwa na mwanafunzi mwingine aliyekosa nafasi.
Orodha ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi mwaka 2015 inapatika hapa. BOFYA  HAPA
 

No comments