Header Ads

Breaking News

MTAA ULIOPEWA JINA LA VICTOR WANYAMA JIJINI DARE ES SALAAM, TANZANIA WAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI

Siku moja baada meya wa Ubungo Boniface Jacob kwa kushirikiana na kamati ya mtaa wa Ubungo kuupa jina la Victor Wanyama mtaa ambao ulikuwa unajulikana kama NHC mtaa huo umezidi kuzua gumzo kwenye mitandao mbalimbali mikubwa duniani.



Mtaa wa NHC kwa sasa umebadilishwa jina na kupewa jina laVictor Wanyama  kiungo wa Tottenham Hotspurs ambaye pia ni nahodha wa timu ya Kenya. hii ni kutokana na ujio  staa huyo katika mtaa huo kushuhudia mechi ya mtaani ya Ndondo Cup kati ya Faru Jeuri dhidi ya Kauzu FC
 
mtaa huo umeripotiwa na mitandao mbalimbali duniani miongoni mwa mitandao hiyo ni pamoja na mtando wa   thesun.co.uk ambao unamilikiwa na News UK. mtandao huu ulianzishwa toka miaka 60  na unawasomaji wengi kutoka sehemu mbalimbali duniani
NINI MAONI YAKO==>>Toa maoni yako hapa chini. usisahau kushare post hii

No comments