KAYA MASIKINI TANZANIA ZAPATIWA BILIONI 440
Serikali leo imesaini makubaliano ya nyongeza ya fedha kwa ajili ya mfuko wa maendelea ya jamii TASAF, makubaliano
ambayo yataifanya benki ya dunia iipatie Tanzania bilioni 440 kwa ajili
ya kupeleka kwenye kaya maskini ikiwa ni chachu ya maendeleo kwa kaya masikini kuwapatia ajira na kuzipa fulsa ya kuwapeleka watoto wao shule na kupata huduma za afya.
Katibu mkuu wa wizara ya fedha Dr. Servacius Likwelile amesaini
mkataba huo kwa niaba ya serikali na kusema kuwa katika mwaka huu wa
fedha mwaka 2015/2016 serikali na benki ya dunia imepitisha miradi 10
ambayo ina thamani ya trilioni 1.9 ambazo zitapelekwa katika miradi
mbalimbali kama kuboresha kilimo, mradi wa kuimarisha umeme vijijini na
elimu.
vs
No comments