ORODHA YA MAJINA YA WATUHUMIWA MAUAJI YA KIBITI
JESHI LA POLISI
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani, Eng. Hamad Yussuf Masauni ametangaza kuwa,
Jeshi la Polisi linawasaka watuhumiwa 16 wa mauaji ambayo yamekuwa
yakiendelea kufanyika katika maeneo ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji mkoani
Pwani kwa muda mrefu sasa.
Hamad Yussuf Masauni
Akitaja
baadhi ya majina ya watuhumiwa hao wanaotafutwa alisema ni pamoja na
Hassan Haruna Kyakalewa Shujaa, kutoka Ikwiriri mwenye umri kati ya
miaka 25-35. Mwingine ni Omari Abdallah Matimbwa.
Wengine
wanaosakwa na jeshi hilo ni, Anafi Rashid Kapera kutoka Kibiti mwenye
miaka kati ya 25-30 mrefu wa wastani, mwenye uso wa mviringo na wa
mwisho ni, Faraji Ismail Nangalava kutoka Kibiti mwenye kati ya miaka
25-35.
Masauni
aliyasema hayo jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo
alisema Jeshi la Polisi lina picha za watuhumiwa wote wanaotafutwa.
Aidha Jeshi la Polisi lilisema kuwa, zawadi nono itatolewa kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahalifu hao.
No comments