LOWASSA: CHADEMA iitishe Kikao cha Kamati Kuu Ili Kujadili Sakata la Viongozi Wake Kukamatwa Mara Kwa Mara
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa ametaka viongozi wa chama
hicho kuitisha kikao cha Kamati Kuu ili kujadili namna ya kudhibiti
vitendo vya kuwakamata viongozi wa chama hicho vinavyofanywa na wakuu wa
mikoa na wilaya.
LOWASSA
Lowassa
ambaye alikuwa waziri mkuu kati ya mwaka 2005 na 2008, alisema hayo
juzi wakati wa futari aliyoindaa kwa madiwani na viongozi wa Chadema na
wakazi wa Dar es Salaam iliyofanyika Mikocheni.
Mwanasiasa
huyo alisema hayo wakati viongozi wa Chadema, akiwamo Waziri Mkuu wa
Serikali ya Awamu ya Tatu, Frederick Sumaye walizuiwa kutembelea miradi
ya maendeleo kwa madai kuwa kabla ya ziara hiyo, Meya wa Ubungo,
Boniface Jacob alifanya kikao cha chama katika jengo la Serikali.
Meya huyo alikamatwa kwa amri ya mkuu wa Wilaya ya Ubungo na kukaa mahabusu kwa saa 48.
Chazo cha habari mpekuzi
No comments