MASHABIKI WA YANGA KUINGIA BURE MECHI YA YANGA NA TP MAZEMBE
UONGOZI wa Klabu ya Yanga umeamua mashabiki watakaoingia uwanjani
kushuhudia mechi kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe, kesho Jumanne
hawatalipa viingilio.
Mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho inayosubiriwa kwa hamu kubwa na
mashabiki wa Yanga, sasa ni bure. Ikiwa hilo litatekelezeka, Yanga
inaweza kupoteza zaidi ya shilingi milioni 300 ambazo zingeweza
kupatikana kutokana na kiingilio cha mchezo huo
Akithibitisha ukweli wa taarifa hiyo mwenyekiti wa klabu ya Yanga alisema
"Kweli viongozi tumekubaliana kwa umoja baada ya kukaa. Tunataka
mashabiki wa Yanga na mashabiki wengine wanaopenda mpira bila kujali ni
wa timu gani wakashuhudie mpira." ==>> Manji:
Pia kuhusu suala la kupoteza pesa nyingi ambazo zingekusanywa kwenye mchezo huo alisema
"Yanga ipo kwa ajili ya wananchi, Yanga ni furaha ya watu wengi".==>> Manji:
pia kuhusu kuingia kwa mashabiki ambao si mashabiki wa yanga alisema
"Mashabiki wa Yanga ni wengi sana Tanzania. Bado hatuamini Wacongo
wanaweza kuwazidi Watanzania kwa wingi. Hata watu wa Simba ni mashabiki
kutoka Tanzania, waende wakaiunge mkono Yanga. Siku moja Yanga watawaunga mkono wao wakiwa wanashiriki michuano ya kimataifa". ==>> Manji
No comments