KOCHA WA YANGA (PLUIJM) ATOA MBINU WATAKAZO ZITUMIA KUWAFUNGA TP MAZEMBE
YANGA imerejea kutoka kambini Antalya, Uturuki huku Kocha Mkuu, Hans
Pluijm akiahidi kuwapa raha mashabiki wa klabu hiyo keshokutwa.
Akizungumza jana, Pluijm alisema kambi ya mazoezi nchini Uturuki
imewajenga na ana matumaini makubwa ya kufanya vizuri Jumanne wakati
Yanga itakapocheza na TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo
(DRC).
“Nawajua TP Mazembe, ni timu nzuri ina wachezaji ambao wamecheza nchi
mbalimbali na baadhi yao nawafahamu nilishawafundisha nikiwa Ghana.
“Mchezo utakuwa mgumu na mzuri, naamini mashabiki pamoja na kuwa
tunasaka pointi tatu, tutawapa burudani, ” ==>> Pluijm.
Alisema wamefanyia kazi udhaifu uliojitokeza katika mchezo wao wa
kwanza na MO Bejaia Jumapili na kwamba ni jukumu la wachezaji kubadilika
kwa kucheza kutokana na maelekezo yake.
Kwa upande wake akizungumza jana, Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro
alisema maandalizi yanaenda vizuri ya mchezo huo na kwambaba kiingilio cha
chini kitakuwa Sh. 7,000 wakati kingilio cha juu ni Sh 30,000.
No comments